Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga anawatangazia Wananchi wote nafasi mbali mbali za kazi kwa watanzania wenyesifa kama ifuatavyo
1. MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III NAFASI 14 – NGAZI YA MSHAHARA NI TGS B
SIFA ZA KUAJIRIWA
- Mwombaji awe na elimu ya Diploma katika moja ya fani zifuatazo Utawala,Sheria,Elimu ya Jamii,Usimamizi wa fedha,Maendeleo ya Jamii,Na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI/MAJUKUMU
i. Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao na kuwa mlinzi wa amani katika mtaa
ii. katibu wa maendeleo ya mtaa
iii. Ataratibu na Kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
iv. Atakuwa Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
v. Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu.
vi. Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na kuongeza uzalishaji mali.
vii. Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya kitaalamu katika kijiji.
viii. Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji.
ix. Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji.
x. Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi.
xi. Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za kijiji.
xii. Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
xiii. Kazi nyingine zote atakazopangiwa na Mwajiri.
2. DEREVA DARAJA LA II MSHAHARA TGOS A NAFASI 1
SIFA ZA KUAJIRIWA
- waombaji wawe na cheti cha mtihani wa kidato cha IV wenye leseni ya Daraja la C ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miatau bila kusababisha ajali, wenye cheti cha majaribio y aufundi Daraja la II kutoka vyuo vya udereva vinavyotambulika na serikali
KAZI NA MAJUKUMU
- kuendesha magari ya abiria na maroli
- kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo unaohitaji matengenezo
- kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari kugundua ubovu
- kufanya matengenezo madogo madogo katika gari
- kutuna log - book kwa safari zote
3. POLISI WASAIDIZI (AUXILIARY POLICE) NAFASI 1
SIFA ZA KUAJIRIWA
-Raia wa Tanzania mwenye umri kati ya miaka 18 na 25, afya njema kiakili na kimwili macho yenye uwezo wa kuona vizuri bila kutumia miwani kwa kiwango cha 6/6R - 6/6L, tabia njema, asiye na kumbukumbu za kupatikana kwa hatia ya makosa ya jinai, uwezo wa kusoma na kuandika kwa kiswahili na kingereza na
- mwenye elimu ya ufahulu wa kidato cha 4 au 6
- mwenye stashahada au shahada kutoka chuo kinachotambulika na Serikali
KAZI NA MAJUKUMU
i/ kulinda na kudmisha usalama wa Halmashauri na mali zake
ii/ kulinda watu na mali zao katika eneo la Halmashauri
iii/ kusimamia utekelezaji wa sheria, kanuni na taratibu
iv/ kufanya doria maeneo mbalimbali ya Halmashauri
v/ kulinda na kusindikiza watuhumiwa kwenda na kurudi kutoka mamlaka husika
vi/ kutuliza fujo inapotokea au tukio lolote linaloashiria uvunjifu wa amani katika eneo la Halmashauri
vii/ kkulinda misafara ya viongozi wanapotembelea maeneo ya Halmashauri
viii/ kuelimisha na kuhamasisha juu ya dhana ya plisi jamii
viii/ kushiriki katika matukio ya dharula pindi yanapojitokea
ix/ kutunza na kuwasilisha vielelezo pindi vinapohitajika
x/ kushiriki kazi za misako katika halmashauri
xi/ kufanya kazi zingine atakazo pangiwa na wakuu wake
4. AFISA MAENDELO YA JAMII MSAIDIZI DARAJA LA II NAFASI 2 MSHAHARA TGS C
SIFA ZA KUAJIRIWA
- Wahitimu wa kidatao cha 4 na 6 wenye stashahada ya maendeleo ya jamii kutoka vyuo vya maendeleo ya jamii (BUHARE & RUNGEMBA) au vyuo vingine vinavyotambulika na serikali
KAZI NA MAJUKUMU
- kuratibu shughuli za maendeleo ya jamii katika kata zikiwemo za wanawake na watoto na za kijisia
- kuwezesha jamii kushiriki katika kubuni na kupanga na kutekeleza kusimamia kuthamini mipango/miradi ya maendeleo
- kuhamasisha na kuwezesha wanachi kupanga na kutekeleza kazi za maendeleo ambazo ni pamoja na usafi wa mazingira, ujenzi wa nyumba bora vijijini, ujenzi wa shule, zahanati, majosho, barabara za vijii na uchimbaji wa visima vifupi na uchimbaji wa marambo
- kuhamasisha na kuwawezesha wananchi kupanga mbinu za kutatua vikwazo vya maendelao hasa maji, na nishati kwa kuwa na miradi ya uvunaji wa maji ya mvua, majiko sanifu namatumizi ya mikokoteni
- kuwa kiungo katika wanakijiji na watumishi wengine wa serikali na kutekeleza shughli za maendeleo
- kuwawezesha wnanchi katika kutekeleza kazi za kujitegemea
- kuwawezesha wananchi kubaini na kuratibu rasilimali zilizopo na kumbukumbu katika miradi ya kujitegemea
- kukusanya na kutunza, kutafsiri na kuwaaidia wananchi kutumia takwimu na kumbukumbu za kijiji
- kuandaa na kutoa taarifa za kazi za maendeleo ya jamii kila mwezi kwa uongozi wa kijiji na kwaafisa maendeleo ya jamii ngazi ya kazta
- kusaidia kuunda vikundi vya kijamii na vya kimaendeleo
- kuratibu shughuli za mashirika na asasi za sizisokuwa za kiserikali na za kijamii
- kuratibu shughuli za kupambana na UKIMWI
5. MPISHI DARAJA LA MM NAFASI 1 MSHAHARA TGS C
SIFA ZA KUAJIRIWA
- wahitimu wa kidato cha 4 waliofuzu mafunzo ya cheti yasipungua mwaka mmoja katika fani ya food production yatolewayo na vyuo vya forodhani (DSM)
Msoka (MOSHI) ARUSHA HOTEL, Y.M.C.A VETA MIKUMI NA VISION HOTEL DSM au vyeti vingine vinayotambuliwa na serikali na wenye uzoefu wa kazi usiopungua miaka mi 3
KAZI NA MAJUKUMU
- kusafisha jiko
- kupika chakula cha kawaida
- kupika vyakula vya aina mbali mbali
- kuhakikisha vyombo vya kupikia vyakula viko safi
6. KATIBU MAHUSUSI DARAJA LA III NAFASI I NGAZI YA MAHSHARA TGSA
SIFA ZA KUAJIRIWA
- waliomaliza elimu ya kidato cha 4 au 6 waliohudhuria mafunzo ya uhazili kutoka chuo cha Utumishi wa Umma au yuo vingine vinavyotambuliwa na serikali na ufahulu mitihani ya ya hatua ya 3 wawe wamefahulu somo la hati mkato ya kiswahili na kingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe mapepata mafunzo ya kumpyuta nakupata cheti katika program za Windows, Microsoft Office, Internet, Email na Publisher
KAZI NA MAJUKUMU
i. kuchapa barua na nyaraka za kawaida
ii. kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu wanayoweza kushughulikiwa
iii. kusaidia kutunza kumbukumbu na taarifa za matukio miadai ya wageni, tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofosi anamofanyia
iv kusaidia kutafuta na kumpatia mkuu wake majalada ya nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo osfisini
v. kusaidia kufikisha maelezo ya mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi ake pia kumwaifu kuhusu taarifa katika shughuli za kzi hapo ofisini
vi. kusaidia kupokea majalada, kuyagawa, kwa maofisa walio katika sehemu alipo na kuyakusanya kuyatunza na kuyarudisha katika sehemu zinazohusika
vi. kutekeleza kazi zote atakazokuwa amepnagiwa na mkuu wake wa kazi
7. FUNDI SANIFU MSAIDIZI NAFASI 1 NGAZI YA MSHARA TGS A
SIFA ZA KUAJIRIWA
Waliomaliza kidato cha 4 katika masomo ya sayansi na kufuzu mafunzo ya mwaka mmoja katika moja ya fani za ufundi kutoka katika chuo kinachotambuliwa na serikali au wenye majaribio ya ufundi hatua ya II chuo cha ufundi katika mojawapo ya fani za ufundi
KAZI NA MAJUKUMU
- atafanya kazi chini ya maelekezo ya mafundi sanifu wa Halmashauri
8. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II NAFASI 1 NGAZI YA MSHAHARA TGS B
SIFA ZA KUAJIRIWA
awe amehitimu kidato cha 4 au 6 wenye cheti cha utunzaji wa kumbukumbu katika moja wapo ya fani za afya, masijala au ardhi
KAZI NA MAJUKUMU
- Kutafuta mafaili/kumbukumbu yanayohitajiwa
- kudhibiti upokeaji na uandikishaji wa nyaraka
-
kuchambua, kuorodhesha na kupanga nyaraka katika makundi kulingana na somo husika kwaajili ya matumzi ya ofisi
- kuweka barua na nyaraka katika mafaili
- kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka taasisi ya Serikali
- kazi nyinginee atakazopangiwa na mkuu wake
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA WAOMBAJI
i. Mwombaji awe Raia wa Tanzania ambaye umri e miaka 18 hadi 45.
ii. maombi yaambatanishwe na vivuli vya vyeti, picha ya passport iliyopigwa hivi karibuni
iii. watumishi waliowahi kuajiriwa serikalini na kupata cheki namba hawataajiriwa tena bali wataajiriwa baada ya kupata kibali cha Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Ummana Utawala Bora
juu ya bahasha andika kazi uliyoomba
iv. provisional results na transcript havitapokelewa
Maombi yatumwe kwa:-
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA JIJI,
S.L.P 178.
TANGA
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 12/09/2017 saa 9:30 alasiri