Breaking

PAKUA MCHAINA APP HAPA CHINI USOME HABARI ZETU HATA USIPOKUWA NA MB

Saturday, September 23, 2017

BREAKING NEWS:RAIS MAGUFULI ATANGAZA NAFASI ZA AJIRA 3000 ZA WANAJESHI



JPM ATANGAZA AJIRA 3,000 ZA JESHI, AJUTA KUWA RAIS

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli ametangaza ajira mpya 3,000 za jeshi ili kuongeza nguvu kazi katika jeshi la wananchi wa Tanzania.

Rais Magufuli ametoa taarifa hiyo wakati akihutubia wakazi wa Arusha waliohudhuiria kushuhudia zoezi la kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa JWTZ 422 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha.


Miongoni mwa mambo aliyozungumza katika hotuba yake, Rais Magufuli amesema anajuta kuwa rais kutokana dosari nyingi alizozikuta karibu kila sehemu ikiwemo ufisadi na wafanyakazi hewa.

Amesema “Nimeamua kuwa sadaka kwa ajili ya kuwanyoosha mafisadi... naamini hapatatokea mwingine atakayejitoa hivi”

Kuhusu Kuhamia Dodoma, amesema mwaka huu makamu wa rais atahamia Dodoma na mwakani yeye mwenyewe atahamia huko huku akionya watakaobaki Dar es Salaam kuwa watakuwa wamejifukuzisha kazi.


ANGALIA VIDEO RAIS AKITAMKA KUTOA AJIRA HAPA CHINI







SOURCE:AZAM TV