BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AWAMU YA PILI YA MAOMBI YA UDAHILI
KWA WAOMBAJI WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA
MWAKA WA MASOMO 2017/2018
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kufahamisha umma kuwa baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya Udahili, awamu ya pili imefunguliwa kuanzia tarehe 18 Septemba, 2017 hadi tarehe 1 Octoba, 2017 kwa vyuo vyote ambavyo bado vina nafasi wazi za udahili.
Hivyo
wahitimu wote wa Elimu ya Sekondari wenye sifa za kujiunga na programu
za Astashahada na Stashahada, walioomba na hawakufanikiwa kupata nafasi
katika awamu ya kwanza na wale ambao hawajaomba hadi
Udahili ulipofungwa tarehe 20 Agosti, 2017 watume maombi ya Udahili
kwenye vyuo vya serikali na binafsi.
Kwa
wanaotaka kuomba vyuo vya Serikali/Umma kwa fani za Ualimu na Afya
watume maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza www.nacte.go.tz kwa kubonyeza kitufe cha Apply online (SAVS) kama
ilivyokuwa awali. Kwa wale ambao wamekweisha fanya maombi kwenye mfumo
na hawakuchaguliwa wanaweza kubadili machaguo yao kwa kurekebisha
programu walizo chaguo au kada kwa kutumia kurasa (Profile) binafsi zao.
Baraza linatoa taarifa kuwa vyuo na
kozi zilizodahili wanafunzi wa kutosha hazitaonekana tena wakati wa
maombi ya awamu hii ya pili. Baraza linapenda kutoa rai kwa waombaji
kuwa wafanye maombi yao mapema ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza
katika dakika za mwisho za kufunga dirisha la Uhakiki.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 20/09/2017