BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)
TAARIFA KWA UMMA
Baraza la
Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuwataarifu Wadau wa Elimu
na Umma kwa ujumla kwamba mafunzo ya Wauguzi Wasaidizi (Nurse
Assistants) na Wahudumu wa Afya (Medical Attendants) si miongoni mwa mafunzo yanayosimamiwa na kutambuliwa na Baraza,
na kwamba chuo chochote kinachotoa na kuendesha mafunzo hayo kinakiuka
Kanuni za Usajili pamoja na Kanuni za Ithibati za Baraza za mwaka 2001.
Kwa
tangazo hili Baraza linawatahadharisha wananchi kwa ujumla kutojiunga na
mafunzo yaliyotajwa hapo juu kwa kuwa tuzo zinazotolewa baada ya
kuhitimu mafunzo hayo pia hazitambuliwi.
Aidha
Baraza linaendelea kufuatilia na kuvibaini vyuo vyote vinavyotoa mafunzo
hayo kwa ajili ya kuchukua hatua stahiki. Kituo au chuo chochote
kitakachokutwa kinatoa mafunzo ya aina hiyo, wahusika watakabidhiwa
kwenye vyombo vya Sheria kwa udanganyifu na kutoa mafunzo
yasiyotambuliwa na Baraza na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia
Wazee na Watoto.
Imetolewa na:
Kaimu Katibu Mtendaji,
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
18/09/2017