Breaking

PAKUA MCHAINA APP HAPA CHINI USOME HABARI ZETU HATA USIPOKUWA NA MB

Friday, February 10, 2017

TAARIFA MPYA KWA UMMA KUTOKA TCU

TAARIFA KWA UMMA

WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA WALIOTHIBITISHWA

KUHAMA PROGRAM AU VYUO




Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwa zoezi la kupokea na kuthibitisha maombi ya uhamisho wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2016/17 limekamilika. Orodha ya wanafunzi waliothibitishwa na TCU imeshawasilishwa kwenye vyuo husika. Hivyo, wanafunzi wote waliotuma maombi ya uhamisho wanaweza kuona matokeo ya uhamisho wao kupitia linki ifuatayo: (BOFYA HAPA KWA INTER UNIVERSITY    na BOFYA HAPA KWA INTERNAL UNIVERSITY)

Hata hivyo, Tume inapenda kuwatangazia wanafunzi wote waliotuma maombi ya uhamisho kwamba:

       Wanafunzi wote waliothibitishwa kuhama vyuo wanatakiwa wawe wamesharipoti kwenye vyuo husika kwa usajili na taratibu nyingine kabla ya muda wa usajili kwisha;

       Wale ambao hawataona majina yao katika orodha ya uhamisho watambue kuwa uhamisho wao haujathibishwa na Tume hivyo wanashauriwa kubaki kwenye vyuo walivyochaguliwa awali;

       Wanafunzi waliohama bila kuidhinishwa hawatatambuliwa na Tume;

       Muda wa kupokea na kuthibitisha maombi ya uhamisho ulikwisha tarehe 18 Desemba, 2016. Hivyo, Tume haipokei tena maombi ya uhamisho toka Taasisi yoyote ya Elimu ya Juu.

       Majina ya wanafunzi wote waliohama yamewasilishwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kwa ajili ya kumbukumbu zake.


Imetolewa na



Katibu Mtendaji

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania 3/1/2017

No comments:

Post a Comment