Wachezaji watano wameteuliwa (NOMINEES) kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2016/2017.
Walioteuliwa kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho ni Aishi Manula (Azam FC), Haruna Niyonzima (Yanga), Mohamed Hussein (Simba), Shiza Kichuya (Simba) na Simon Msuva (Yanga).
Majina hayo yatapigiwa kura na makocha, makocha wasaidizi na manahodha
wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na wahariri wa michezo kutoka
vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Wahusika watatumiwa fomu maalum za kupiga kura kwenye email za klabu zao
na vyombo husika vya habari. Mwisho wa kupiga kura ni saa 6 usiku ya
Jumanne, Mei 23 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment