Na Baltazar Mashaka, Mwanza
SERIKALI mkoani Mwanza imewataka waumini wa madhehebu ya dini mbalimbali humu na kote nchini kudumisha umoja, mshikamano na utulivu Tanzania iendelee kuwa kisiwa cha amani.
Kauli
hiyo ilitolewa juzi (jana) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella
(wa pili kushoto pichani) wakati wa Maulid iliyofanyika kwenye Uwanja
wa Shule ya Msingi Mbugani katika Wilaya ya Nyamagana jijini hapa.
Alisema
kuwa dini zote msingi wake ni amani, kusamehe, kuvumiliana na
kushirikiana wananchi na waumini wa dini zote wakiyataimiza hayo nchi
itaendelea kuwa kisiwa cha amani.
“Mikusanyiko
kama hii inachangia shughuli za serikali maana yanazungumza amani
lakini mengine ni shida.Natamani watanzania leo wangeyasikia ama
wakiyasikia na kuyachukua haya nchi itakuwa na amani,”alisema Mongella
huku akiweka bayana kuwa yeye ni mnazi wa Simba lakini aliwakabidhi
Kombe Yanga kwa amani.
Alidai
kuwa kazi bado ni kubwa na kinachotakiwa ni kuwapa wananchi moyo
kutokana na kauli mbiu ya Maulid hayo kusistiza umoja, utii wa sheria na
ushirikiano na kueleza kuwa hata Aya zilizokuwa zikitolewa hapo amekuwa
akizisikia hata kwa Mapadri.
Mkuu
huyo wa mkoa alisistiza kuwa nchini itaendelea kuwa kisima cha amani na
utulivu kama jamii itakuwa tayari kutimiza matakwa ya dini ambayo
msingi wake ni amani , kusameheana, kuvumiliana na kushirikiana.
Pia
Mongella alisema serikali inaheshimu kazi zinazofanywa na Baraza kuu la
Waislamu Tanzania (BAKWATA) na ndicho chombo inachofanya kazi nacho,
naitaendelea kushirikiana kwa maendeleo ya mkoa na taifa maana haitapa shida kutoka kwao licha ya mifumo iliyopo.
Aidha, Kaimu Mufti wa Tanzania Sheikh Othman Issa Othman aliwaonya
waumini wa dini ya kiislamu kuwa Mungu amewapa mtihani na hivyo
wasizitumie simu za kisasa kufanya vitu haramu na kuvifanya siri, ipo
siku vitakuwa hadharani.
“Mwaka
huu wa Hijiria tujiandae na mfungo mtukufu wa mwezi Ramadhan.Tunaweza
kufanya mambo ya ovyo, ili tutambue Mungu katupa mtihani, mtihani huo
anataka kufahamu nani anamwoga kwa siri.Tuzitumie vizuri simu za Smart
Phone mamana hata tukiweka namba za siri iko siku hayatakuwa siri
tena,”alisema kaimu Mufti.
Alisema mwenyezi Mungu kawapa Maswahaba wake mtihani ili wavuke na kuwataka wajiandae na mfungo wa mwezi Ramadhan, hivyo wazitumie simu hizo kutengeneza makundi ya swala za alfajiri ili kukumbushana ya kheri badala yale ya ovyo yasiyompendeza mwenyezi Mungu.
Awali Mwenyekiti wa Jumuiya
ya Kuendeleza Quraan na Sunna Tanzania (JUQUSUTA) yenye makao yake
jijini Mwanza iliyoandaa Maulid hayo , Sheikh Hassan Kabeke alisema
kauli mbiu yake ni kujenga maadili mema, amani na utulivu, kupinga
vitendo viovu vya uvunjifu wa amani na utii wa sheria bila shuruti.
No comments:
Post a Comment