Timo Werner (kulia), mfungaji wa mabao mawili ya Ujerumani dakika za 66 na 81 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Cameroon leo Uwanja wa Olimpiki
Fisht mjini Sochi, Urusi kwenye mchezo wa Kundi B Kombe la Mabara
akimiliki mpira dhidi ya dhidi ya beki wa Simba Wasiofungika, Adolphe
Teikeu (kushoto). Bao lingine la Ujerumani limefungwa na Kerem
Demirbay dakika ya 48, wakati la Cameroon limefungwa na Vincent
Aboubakar. Kwa matokeo hayo, Cameroon inatolewa kwenye mashindano, huku
Ujerumani ikienda Nusu Fainali
No comments:
Post a Comment