Breaking

PAKUA MCHAINA APP HAPA CHINI USOME HABARI ZETU HATA USIPOKUWA NA MB

Monday, July 3, 2017

ASTON VILLA WAMNYAKUA RASMI JOHN TERRY




Aliyekuwa nahodha wa Chelsea, John Terry amejiunga rasmi na Klabu ya Aston Villa inayoshiriki Ligi daraja la kwanza ‘Championship.’

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaonyesha kuwa tayari beki huyo mwenye umri wa miaka 37 aliyedumu na Chelsea kwa miaka 22, amekwisha saini kuitumikia klabu hiyo iliyomaliza msimu uliopita ikiwa nafasi ya 13.

Mmiliki wa klabu hiyo yenye makazi yake Villa Park pamoja na Mwenyekiti wake Dkt. Tony Xia ndiyo waliothibitisha kuwasili kwa gwiji mkongwe huyo klabuni hapo kupitia mtandao wa twitter.

Dkt. Tony ameandika “Karibu JT katika Jiji la Birmingham…. Aston Villa, taarifa rasmi inakuja punde,” Kauli inayoashiria ujio wa Terry klabuni hapo.

Aston Villa kumnasa Terry katika kipindi hiki, ni sawa na pigo kwa mahasimu wao, Birmingham City, ambao pia walikuwa wakimfukuzia beki huyo aliyetwaa mataji 17 akiwa na Chelsea yakiwemo matano ya EPL.

Terry amekuwa na lengo la kutafuta changamoto mpya katika makazi mengine, na hivyo kufikia makubaliano ya kuachana na Chelsea, ambapo alifanyiwa hafla ya kuagwa rasmi klabuni hapo katika mchezo wa kuhitimisha msimu uliopita wa Ligi Kuu ya England.

No comments:

Post a Comment