Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Hassan Abbasi.
Mkurugenzi wa Habari Maelezo Dkt.
Hassan Abbasi amefunguka na kusema hakuna chombo cha habari ambacho
kitachukuliwa hatua na serikali kwa kuandika habari zenye mrengo wa
kukosoa sera na utekelezaji wake na kusema watu wamekuwa wakipotosha
umma.
Dkt. Abbasi amesema kuwa Sheria na 12 ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
kifungu cha 51 kinatoa ruhusa kwa chombo cha habari kukosoa kwa lengo la
kuonyesha njia mbadala katika kutatua changamoto zinazowakabili
wananchi.
“Hakuna chombo cha habari kitakachochukuliwa hatua kwa kukosoa, haki
hiyo ipo kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 kifungu
cha 51, tutaendelea kuthamini na kufanyia kazi ukosoaji huo,” alisema
Dkt. Abbasi.
Mbali na hilo Dkt. Hassan Abbasi amedai kuwa kama serikali haitasita
kuvichukulia hatua vyombo vya habari vyote ambavyo vitakiuka sheria na
misingi ya maadili ya taaluma ya habari kwa lengo la kulinda maslahi ya
taifa.
Dkt. Abbasi alisitiza kuwa ni vyema wamiliki wa vyombo vya habari
wakatumia uhuru huo wa kisheria kuchapisha habari zenye nia njema kwa
mustakabali wa maendeleo ya nchi badala ya kueneza hofu miongoni ya mwa
jamii.
No comments:
Post a Comment