Breaking

PAKUA MCHAINA APP HAPA CHINI USOME HABARI ZETU HATA USIPOKUWA NA MB

Wednesday, July 5, 2017

BREAKING NEWS:MABADILIKO AJIRA ZA TRA HAYA HAPA ANGALIA HAPA

MABADILIKO KATIKA TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA TRA (Kumb. Na. EA.7/96/01/148)
 July 5, 2017.

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwapa taarifa wadau wetu hususan waombaji kazi waliokuwa wameshawasilisha maombi na wale ambao watapenda kuwasilisha maombi ya kazi kwa nafasi zilizotangazwa na chombo hiki kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuwa kuna mabadiliko yamefanywa na mamlaka husika (TRA) ambapo nafasi za kazi mia moja (100) zilizokuwa zikiwahitaji (ESTATE OFFICER II) hazitakuwepo tena na badala yake watahitajika (REVENUE OFFICER II -100).

Hivyo, wale waombaji ambao walikwishawasilisha maombi yao kwa nafasi hiyo, watapaswa kuyawasilisha upya na kuzingatia sifa zilizoainishwa katika tangazo lenye Kumbukumbu namba EA.7/96/01/149 lililoko kwenye tovuti www.ajira.go.tz ambalo mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 19 Julai, 2017.

Tunapenda kuwaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaokuwa umejitokeza kutokana na mabadiliko hayo.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Sekretarieti ya Ajira

No comments:

Post a Comment